Thawabu anazokosa anayejitwahirisha msikitini badala ya nyumbani

Swali: Ni ipi hukumu ya yule anayetoka nyumbani kwake hali ya kuwa na twahara ambapo kila hatua moja inamwandikia jema na hatua nyingine inamfutia dhambi au maana inayofanana na hiyo? Unasemaje kwa yule aliyetoka hali ya kutokuwa na twahara na akajitwahirisha msikitini?

Jibu: Kilicho bora zaidi ni ajitwahirishe nyumbani kwake, kama ilivyokuja katika Hadiyth. Anapotoka nyumbani kwake hali ya kuwa na twahara, basi Allaah humwandikia kwa kila hatua; hatua ambayo Allaah anamnyanyua kwa ajili yake ngazi na hatua nyingine inamfutia dhambi na kumwandikia jema mpaka afike msikitini. Huendelea kuwa katika hukumu ya swalah muda wa kuwa anasubiri swalah.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31701/ما-الاجر-المترتب-لمن-يخرج-من-بيته-متطهرا
  • Imechapishwa: 16/11/2025