Swali: Unasemaje kuhusu maneno ya Fudhwayl kwamba anayeacha kutenda kwa ajili ya watu amefanya shirki?

Jibu: Maneno ya Fudhwayl hayatumiki katika hali zote. Maneno ya Fudhwayl hayatumiki katika hali zote.

Swali: Aache?

Jibu: Hakuna ubaya. Nakusudia kwamba asiache kutenda kwa ajili ya watu. Afanye yale ambayo Allaah amemuwekea katika Shari´ah na asiwajali watu. Lakini asikusudie kuwaonyesha katika matendo yake. Ama kusema kwamba anaacha matendo ili asiambiwe kuwa anajionyesha, hapana. Aswali na asiwajali. Aswali Dhuhaa na swalah zingine za kujitolea na asijali. Aswali swalah za usiku na wala asijali ijapo watasema kuwa anajionyesha. Hayamdhuru maneno ya watu muda wa kuwa Allaah anajua kuwa ametakasika na jambo hilo na kusudio lake sio kujionyesha.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24635/حكم-ترك-العمل-لاجل-الناس-خشية-الرياء
  • Imechapishwa: 16/11/2024