Tayammum kwa ambaye yuko na maji kidogo

Swali: Ikiwa mtu atapata maji jangwani lakini hayatoshi kutawadhia, je, inajuzu kutumia udongo kwa ajili ya Tayammum?

Jibu: Atumie maji yaliyopo kwa viungo vinavyotosheka, kisha atayamamu kwa ajili ya viungo vilivyobaki. Allaah (Ta´ala) amesema:

فَاتَّقُوا اللَّـهَ مَا اسْتَطَعْتُمْ

”Mcheni Allaah muwezavyo.”[1]

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Pindi nitakapokuamrisheni jambo lolote, basi lifanyeni kwa kadiri ya uwezo wenu.”[2]

Kuna maafikiano juu ya usahihi wake.

[1] 64:16

[2] al-Bukhaariy (13/251) na Muslim (04/1830).

  • Muhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (5/337-338)
  • Imechapishwa: 26/11/2026