Maji baridi au ya moto wakati wa kuoga janaba?

Swali: Ni maji gani yanayofaa zaidi kwa mtu kutumia wakati wa kuoga janaba, maji baridi au maji ya moto? Je, afanye nini mtu ambaye hawezi kutumia maji baridi?

Jibu: Muislamu anaweza kutumia maji ya moto au maji baridi kulingana na maslahi yake. Jambo hili ni lenye wasaa. Dini ya Allaah ni nyepesi. Amesema (Subnaanah):

يُرِيدُ اللَّـهُ بِكُمُ الْيُسْرَ وَلَا يُرِيدُ بِكُمُ الْعُسْرَ

”Allaah anakutakieni mepesi na wala hakutakieni magumu.”[1]

[1] 02:185

  • Muhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (5/327)
  • Imechapishwa: 26/11/2026