Tayammum inachukua nafasi ya wudhuu´

Swali: Je, ni sahihi kuswali swalah nyingi za faradhi kwa Tayammum au ni lazima mtu kufanya Tayammum juu ya kila swalah?

Jibu: Allaah (Ta´ala) amefanya Tayammum badala ya kutawadha. Yale yaliyojuzishwa kufanywa baada ya kutawadha yanafaa kufanywa baada ya Tayammum. Ni kweli kuna Hadiyth inayosema kuwa mtu asiswali kwa Tayammum isipokuwa tu swalah moja, lakini ni dhaifu. Kwa hivyo inafaa kuswali swalah nyingi kwa Tayammum moja.

  • Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Qam´-ul-Mu´aanid, uk. 300-301
  • Imechapishwa: 09/01/2025