Swali: Katika mji wetu watu wanatufu kwenye makaburi na wanaapa kwa asiyekuwa Allaah kwa madai ya kwamba Tawhiyd ni kwa nia. Ni ipi njia bora zaidi ya kuwakinaisha hawa wanaoapa kwa asiyekuwa Allaah kwa madai ya kwamba Tawhiyd ni kwa nia? Vipi nitawakinaisha?

Jibu: Tawhiyd ni kwa nia na vipi kuhusu kitendo? Je, Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikubali nia za Maswahabah? Bali kinyume chake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliwapiga vita washirikina. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Nimeamrishwa kuwapiga watu vita mpaka waseme ´hapana mola wa haki isipokuwa Allaah`.”

Katika Hadiyth ya Mu´aadh wakati Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipomtuma akamwambia:

“Iwe jambo la kwanza utakalowalingania kwalo ´nashuhudia ya kwamba hapana mola wa haki isipokuwa Allaah`.”

Katika upokezi mwingine:

“…. wampwekeshe Allaah.”

Ni lazima Tawhiyd ipatikane kwa maneno na vitendo. Nia peke yake haitoshelezi.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajhiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://subulsalam.com/play.php?catsmktba=11649
  • Imechapishwa: 01/05/2015