Swali: Je, ni sharti swalah ya Witr kutoa Tasliym mbili au inatosha kutoa Tasliym moja?
Jibu: Ni Tasliym mbili kama swalah zingine. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akileta Tasliym mbili katika swalah zinazopendeza na swalah za faradhi.
Mwendesha kipindi: Kwa hivyo aswali Rak´ah mbili, alete Tasliym, kisha alete Rak´ah moja?
Jibu: Ndio, hivi ndio Sunnah na bora. Ni sawa pia akiswali zote tatu kwa pamoja.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/10857/كيفية-التسليم-بعد-صلاة-الوتر
- Imechapishwa: 08/04/2023