Swali: Tuko katika msimu wa baridi. Maimamu wanakusanya kati ya Maghrib na ´Ishaa pindi kunapotimia zile sababu zinazoruhusu kukusanya swalah. Tunakaribia mwezi wa Ramadhaan. Je, inafaa kuswali Tarawiyh baada ya swalah ya ´Ishaa ikikusanywa na Maghrib katika wakati wa swalah ya Maghrib?

Jibu: Hapana vibaya kuswali Tarawiyh baada ya swalah ya ´Ishaa mnapokusanya na Maghrib kwa sababu ya udhuru unaokubalika katika Shari´ah kukusanya kwa sababu ya kutokuwa kipingamizi ya kufanya hivo.

´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz

´Abdullaah bin Ghudayyaan

Swaalih al-Fawzaan

´Abdul-´Aziyz Aalish-Shaykh

Bakr Abu Zayd

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Lajnah ad-Daaimah nr. (16977)
  • Imechapishwa: 22/04/2022