Swali: Ilitokea siku ya ´Arafah na katika msikiti wa ´Urnah kwamba mtu mmoja alianza kutamka Talbiyah kwa kutumia vipaza sauti, kisha watu wote wakawa wakitamka Talbiyah nyuma yake. Kitendo hiki kikaendelea mara kadhaa. Je, jambo hili linajuzu? Kwa maana kutamka Talbiyah kwa namna hiyo? Ikiwa hakijuzu, tunaomba kutolewe onyo kuhusu hilo siku zijazo.
Jibu: Talbiyah imesuniwa kwa wote; kila mmoja hutamka Talbiyah peke yake. Ama mtu kutamka kwa kipaza sauti kwa lengo la kuwakumbusha watu na kuwahamasisha, si kwa lengo la Takbiyr ya pamoja, wala Talbiyah ya pamoja, basi kutoa kumbusho kwa kipaza sauti wakati watu wameghafilika ili wasikie, hakuna tatizo katika hilo. Lakini isiwe Talbiyah ya pamoja kwa sauti za pamoja, hapana.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/2576/حكم-التلبية-بمكبرات-الصوت
- Imechapishwa: 28/03/2026
Swali: Ilitokea siku ya ´Arafah na katika msikiti wa ´Urnah kwamba mtu mmoja alianza kutamka Talbiyah kwa kutumia vipaza sauti, kisha watu wote wakawa wakitamka Talbiyah nyuma yake. Kitendo hiki kikaendelea mara kadhaa. Je, jambo hili linajuzu? Kwa maana kutamka Talbiyah kwa namna hiyo? Ikiwa hakijuzu, tunaomba kutolewe onyo kuhusu hilo siku zijazo.
Jibu: Talbiyah imesuniwa kwa wote; kila mmoja hutamka Talbiyah peke yake. Ama mtu kutamka kwa kipaza sauti kwa lengo la kuwakumbusha watu na kuwahamasisha, si kwa lengo la Takbiyr ya pamoja, wala Talbiyah ya pamoja, basi kutoa kumbusho kwa kipaza sauti wakati watu wameghafilika ili wasikie, hakuna tatizo katika hilo. Lakini isiwe Talbiyah ya pamoja kwa sauti za pamoja, hapana.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/2576/حكم-التلبية-بمكبرات-الصوت
Imechapishwa: 28/03/2026
https://firqatunnajia.com/talbiyah-za-pamoja/