Swali: Je, talaka inapita ikiwa amemwacha kwa talaka ya kizushi?
Jibu: Wanazuoni wametofautiana kuhusu talaka ya kizushi kama inapita au haupiti. Wengi wa wanazuoni wameona kuwa inapita. Wengi wa wanazuoni wameona kuwa kizushi pamoja na kuwa ni haramu. Kundi la wanazuoni wengine wakaona kuwa haipiti, msimamo ambao umechaguliwa na kundi katika Salaf, pia imenukuliwa kutoka kwa Ibn ´Umar, Twaawuus bin Kiysaan al-Yamaniy mwanafunzi mtukufu wa Maswahabah na kutoka kwa Khallaad bin ´Amr mwanafunzi mtukufu wa Maswahabah. Ndio maoni pia yaliyochaguliwa na Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah na Ibn-ul-Qayyim na jopo. Wamesema kwa sababu imetokea kinyume cha amri ya Allaah, hivyo basi haipiti. Wengi wamesema kuwa amefanya kosa, ametenda vibaya na inatekelezwa juu yake, kwa sababu Ibn ´Umar alihesabu talaka yake aliyoitoa ndani ya hedhi. Aliihesabu na akaifanya ifanye kazi juu yake hali ya kuhesabiwa juu yake talaka moja. Lakini haikuthibiti kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliihesabu juu yake, lakini yeye aliizingatia na akaifanya ifanye kazi juu yake kwa dhahiri ya maandishi yaliyokuja kutoka kwake. Ameulizwa katika riwaya kutoka kwake kuhusu mtu aliyempa talaka mke wake wakati wa hedhi ambapo akajibu kwamba haihesabiwi. Hili ni katika yanayobainisha kwamba alihesabu talaka yake aliyotoa katika hedhi kwa jitihada yake. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimwambia:
”Mrejee, kisha umshike mpaka atwaharike, kisha apatwe na hedhi, kisha atwaharike, kisha ukitaka basi mtaliki na ukitaka basi mshike.”
Lau talaka hiyo ingekuwa imepita, basi makusudio yangekuwa kuongeza talaka.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1276/حكم-ايقاع-الطلاق-البدعي
- Imechapishwa: 14/02/2026
Swali: Je, talaka inapita ikiwa amemwacha kwa talaka ya kizushi?
Jibu: Wanazuoni wametofautiana kuhusu talaka ya kizushi kama inapita au haupiti. Wengi wa wanazuoni wameona kuwa inapita. Wengi wa wanazuoni wameona kuwa kizushi pamoja na kuwa ni haramu. Kundi la wanazuoni wengine wakaona kuwa haipiti, msimamo ambao umechaguliwa na kundi katika Salaf, pia imenukuliwa kutoka kwa Ibn ´Umar, Twaawuus bin Kiysaan al-Yamaniy mwanafunzi mtukufu wa Maswahabah na kutoka kwa Khallaad bin ´Amr mwanafunzi mtukufu wa Maswahabah. Ndio maoni pia yaliyochaguliwa na Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah na Ibn-ul-Qayyim na jopo. Wamesema kwa sababu imetokea kinyume cha amri ya Allaah, hivyo basi haipiti. Wengi wamesema kuwa amefanya kosa, ametenda vibaya na inatekelezwa juu yake, kwa sababu Ibn ´Umar alihesabu talaka yake aliyoitoa ndani ya hedhi. Aliihesabu na akaifanya ifanye kazi juu yake hali ya kuhesabiwa juu yake talaka moja. Lakini haikuthibiti kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliihesabu juu yake, lakini yeye aliizingatia na akaifanya ifanye kazi juu yake kwa dhahiri ya maandishi yaliyokuja kutoka kwake. Ameulizwa katika riwaya kutoka kwake kuhusu mtu aliyempa talaka mke wake wakati wa hedhi ambapo akajibu kwamba haihesabiwi. Hili ni katika yanayobainisha kwamba alihesabu talaka yake aliyotoa katika hedhi kwa jitihada yake. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimwambia:
”Mrejee, kisha umshike mpaka atwaharike, kisha apatwe na hedhi, kisha atwaharike, kisha ukitaka basi mtaliki na ukitaka basi mshike.”
Lau talaka hiyo ingekuwa imepita, basi makusudio yangekuwa kuongeza talaka.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1276/حكم-ايقاع-الطلاق-البدعي
Imechapishwa: 14/02/2026
https://firqatunnajia.com/talaka-ya-kizushi-inapita/
Mshirikishe mwenzako:
- Share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Print (Opens in new window) Print
- Email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Share on X (Opens in new window) X
- Share on Pocket (Opens in new window) Pocket