Swali: Je, inajuzu haki ya talaka iwe mikononi mwa mwanamke?

Jibu: Hili halifai. Haki ya talaka iko mikononi mwa mume. Ikiwa mume atamkabidhi mwanamke haki hiyo moja kwa moja kuwa mikononi mwake, basi hiyo inakuwa ni sharti batili. Kama ndoa itafungwa kwa sharti hilo, sharti hilo ni batili. Ama kuhusu uwakala, ikiwa mume atamwakilisha mke wake katika baadhi ya nyakati maalum, basi hilo halina tatizo.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/2119/حكم-جعل-العصمة-بيد-المراة
  • Imechapishwa: 02/01/2026