Swali 881: Inajuzu kumtaliki mke mjamzito?

Jibu: Kumtaliki mwanamke mwenye mimba hakuna neno. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisema kumwambia ´Abdullaah bin ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa) wakati alipomtaliki mke wake akiwa na hedhi:

“Mrejee. Kisha mzuie mpaka atwaharike, kisha apate hedhi, kisha apate hedhi, kisha mtaliki ukitaka akiwa msafi kabla ya kumjamii au akiwa mjamzito.”

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Mar´ah al-Muslimah, uk. 352
  • Imechapishwa: 27/07/2019