Swali: Je, talaka inapita kwa maneno yasiyo ya wazi, kama mwanaume akisema ”Nenda kwa watu wako” huku akiwa anakusudia talaka?

Jibu: Ndiyo, talaka inapita kwa maneno ya kinaya ikiwa atakuwa amekusudia talaka. Akisema ”Jiunge na watu wako, ”Nenda kwa watu wako” au ”Rudi kwa watu wako” naye akakusudia talaka, basi talaka inapita na hutokea talaka moja.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/2126/حكم-الطلاق-بالكنايات
  • Imechapishwa: 02/01/2026