Tajiri msafiri kupewa fungu la zakaah kwa kupoteza mali yake

Swali: Lau mtu ni msafiri na mali yake ikapotea au ikaibiwa na katika mji wake ni mtu tajiri. Hawezi kufika katika mji wake na mali alionayo kutokana na uzito au kwa sababu benki zimefungwa. Je, anaweza kupewa anachokihitajia katika Zakaah kiwango kitachomfikisha kwa familia yake?

Jibu: Ndio, hakuna neno. Huyu ni mpita njia. Huyu ni mpita njia ambaye matumizi yake ima yamekwisha, yamepotea au yameibiwa na hana uwezo wa kutumia mali yake. Afanye nini? Wamuache afe au awaombe watu? Apewe. Huyu ni mpita njia.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (13) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo–1431-1-24.mp3
  • Imechapishwa: 11/11/2014