Swali: Ni yepi maoni yenu kuhusu mtu aliyoulizwa juu ya nguo inayovuka vifundo vya miguu na akasema kuwa hicho ni kiburi. Je, hilo linahesabika kuwa ni tafsiri au ni kubadilisha maneno ya Mtume? Ni ipi hukumu?
Jibu: Kuvaa nguo inayovuka vifundo vya miguu ni njia inayopelekea kiburi, siyo kiburi chenyewe. Lakini kwa kawaida huwa ni njia yake. Mara nyingi humpelekea mtu kwenye kiburi. Ama kusema kwamba kuburuta nguo ndiyo kiburi kwa dhati yake, hapana. Bali ni njia ya kufikia kiburi na ni mlango unaoelekea huko. Kwa sababu hiyo Uislamu umeiharamisha na ukaikataza, kwa kuwa ni njia inayopelekea kiburi. Pia ni sababu ya kuharibu nguo, kuzitia najisi, kuzichafua na kuzifanya zipotee. Pale ´Umar (Radhiya Allaahu ´anh) alipomuona kijana mmoja nguo yake ikigusa ardhi alimwambia:
”Ee ´Abdullaah, inua nguo yako! Kwa sababu hilo ni uchaji zaidi kwa Mola wako na ni usafi zaidi kwa nguo yako.”
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1707/ما-حكم-الاسبال
- Imechapishwa: 03/07/2026
Swali: Ni yepi maoni yenu kuhusu mtu aliyoulizwa juu ya nguo inayovuka vifundo vya miguu na akasema kuwa hicho ni kiburi. Je, hilo linahesabika kuwa ni tafsiri au ni kubadilisha maneno ya Mtume? Ni ipi hukumu?
Jibu: Kuvaa nguo inayovuka vifundo vya miguu ni njia inayopelekea kiburi, siyo kiburi chenyewe. Lakini kwa kawaida huwa ni njia yake. Mara nyingi humpelekea mtu kwenye kiburi. Ama kusema kwamba kuburuta nguo ndiyo kiburi kwa dhati yake, hapana. Bali ni njia ya kufikia kiburi na ni mlango unaoelekea huko. Kwa sababu hiyo Uislamu umeiharamisha na ukaikataza, kwa kuwa ni njia inayopelekea kiburi. Pia ni sababu ya kuharibu nguo, kuzitia najisi, kuzichafua na kuzifanya zipotee. Pale ´Umar (Radhiya Allaahu ´anh) alipomuona kijana mmoja nguo yake ikigusa ardhi alimwambia:
”Ee ´Abdullaah, inua nguo yako! Kwa sababu hilo ni uchaji zaidi kwa Mola wako na ni usafi zaidi kwa nguo yako.”
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1707/ما-حكم-الاسبال
Imechapishwa: 03/07/2026
https://firqatunnajia.com/tafsiri-ya-isbaal/