Swawm ya siku sita za Shawwaal pamoja na nia ya masiku meupe

Swali: Je, ni bora kufunga siku sita za Shawwaal kwa kufululiza kuliko kuzitenganisha?

Jibu: Ndiyo, kufululiza. Bora ni kufunga siku sita hizo kwa kufululiza kwa sababu ni kukimbilia katika kheri.

Swali: Je, anapata ujira akifunga siku sita pamoja na masiku meupe yaliyoangukia  jumatatu na alkhamisi?

Jibu: Akinua siku sita anapata ujira wake.

Swali: Pamoja na masiku meupe?

Jibu: Hapana, ana malipo ya siku sita alizonuia.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24664/هل-التتابع-افضل-في-صيام-ست-شوال
  • Imechapishwa: 22/11/2024