Swali: Yule anayekula ribaa katika mwezi wa Ramadhaan. Je, swawm yake inakubaliwa?

Jibu: Ribaa ni haramu katika Ramadhaan na nje ya Ramadhaan. Ni haramu kula ribaa katika Ramadhaan na nje yake.

Swali: Je, swawm yake inakubaliwa?

Ibn Baaz: Inatarajiwa kukubaliwa, lakini yuko katika khatari ya maasi.

Swali: Katika baadhi ya maduka Ulaya wamiliki wake ni waislamu na Ramadhaan wanauza pombe na nyama ya nguruwe.

Ibn Baaz: Ni lazima kuchukua tahadhari na wakemewe. Wafundishwe kwamba jambo hili kwamba ni haramu na ni dhambi ili wajifunze na wanufaike na waache hayo.

Swali: Lakini hilo haliingii katika swawm?

Ibn Baaz: Hapana, swawm inaingia dosari. Lakini haibatiliki. Haibatiliki swawm isipokuwa kwa mambo yanayovunja swawm. Lakini kufanya maasi kunaipunguza swawm na kunapunguza thawabu na malipo yake.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/30898/ما-حكم-صيام-اكل-الربا-وباىع-الخمر
  • Imechapishwa: 15/09/2025