Swali: Je, kuangalia televisheni au yanayorushwa na setilaiti au yanayoonyeshwa kwenye madishi yanaipunguza swawm?

Jibu: Hayo ni maovu. Kuangalia filamu chafu kwenye televisheni au madishi haijuzu kwa mwenye kufunga wala asiyefunga. Hata hivyo hakubatilishi swawm. Kuangalia maovu hakubatilishi swawm, lakini mtu anapata dhambi. Ni mamoja iwe ni kwenye dishi, televisheni au mikononi mwa watu waliokaa.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/25433/ما-حكم-مشاهدة-المنكرات-اثناء-الصيام
  • Imechapishwa: 19/03/2025