Swali: Mwanamke amesibiwa na maradhi ya kupatwa na jini kabla ya Ramadhaan. Ilipofika Ramadhaan ikawa anazimia kuanzia alfajiri mpaka baada ya magharibi na wakati mwingine muda kidogo kabla ya magharibi kwa saa moja au mfano wake. Ni vipi atazilipa siku hizo?

Jibu: Ikiwa kuzimia kunamchukua siku nzima muda kidogo kabla ya kuchomoza kwa alfajiri mpaka kuzama kwa jua, basi anapaswa kulipa siku hiyo. Lakini yakimpata baada ya kuchomoza kwa alfajiri basi funga yake ni sahihi ikiwa hayakumwendelea kwa muda wa siku mbili au tatu. Ama ikiwa yamempata sehemu tu ya siku ni jambo lisilomdhuru. Kwa sababu ni kama mfano wa kulala. Lakini ikiwa ni kwa kipindi cha siku nzima basi atatakiwa kuilipa siku ambayo ana uchangamfu na siku ambayo ana uwezo. Wakati [wa Ramadhaan] ni mpana.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (17)
  • Imechapishwa: 20/09/2020