Swali: Siku ya jumatatu ikiafikiana na siku miongoni mwa masiku meupe au kafara ya kiapo; je, inafaa kwangu kuweka nia ya kufunga swawm ya sunnah ya jumatatu, siku moja wapo ya masiku meupe au kafara ya kiapo?

Jibu: Ikiwa funga ni ya lazima basi ni lazima kunuia kufunga swawm hiyo ya lazima. Ama ikiwa funga zote mbili ni za sunnah, kama funga ya jumatatu ikaangukia katika masiku meupe, basi malengo yanafikiwa kwa nia hiyohiyo moja – na himdi zote njema ni stahiki ya Allaah. Lakini ikiwa ni ulipaji wa swawm ya lazima basi ni lazima kutia nia ya swawm hiyo ya lazima, ni mamoja ni funga ya jumatatu au nyengine. Katika hali hiyo mtu atalazimika kufunga kwanza swawm hiyo ya lazima kabla ya kuanza kufunga swawm iliyopendekezwa. Ikiwa mwanamme au mwanamke analazimika kulipa funga ya lazima, basi anatakiwa kuanza nayo kabla ya kuingia katika swawm ya sunnah.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/15441/حكم-جمع-اكثر-من-نية-في-الصوم-الواحد
  • Imechapishwa: 26/05/2021