Swalah za kujitolea bora ni kuziswali nyumbani hata Makkah

Swali: Swalah inayopendeza ni bora kwa hali zote hata ikiwa ni Makkah?

Jibu: Hata ikiwa ni Makkah. Makkah yote mtu analipwa swalah yake maradufu.

Swali: Anaweza kuswali nyumbani pia?

Jibu: Ndio.

Swali: Hilo halikusanyi Tarawiyh?

Jibu: Hilo linakusanya vyote. Lakini hilo ilikuwa katika uhai wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), kwa sababu alikhofia wasije kufaradhishiwa nayo. Baada ya kufariki kukaaminika kutofaradhishwa.