Swalah ya pamoja wakati wa kupatwa kwa jua na swalah ya ´Iyd

Swali: Swalah ya kupatwa kwa jua na mwezi na swalah ya ´Iyd mbili zinanadiwa kwa kusema (الصلاة جامعة)?

Jibu: Swalah ya kupatwa kwa jua ndiyo inanadiwa kwa kusema hivo pekee. Ama ´Iyd mbili, hapana. Hazina Iqaaamah wala adhaana. Ni kupatwa kwa jua tu  ndio inanadiwa kwa kusema (الصلاة جامعة). Ama swalah ya ´Iyd haina tangazo lolote wala (الصلاة جامعة) wala kitu kingine. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akiswali bila adhaana wala Iqaamah. Swalah ya ´Iyd na ya kuomba mvua zinajulikana. Hazihitaji adhaana.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31550/حكم-قول-الصلاة-جامعة-في-الكسوف-والعيدين
  • Imechapishwa: 02/11/2025