´Allaamah ar-Raajihiy: Adhaana ni wajibu kwa kila msikiti au inatosha ikiwa kumeadhiniwa katika mji?

Jibu: Ni kwa kila msikiti, ndio.

´Allaamah ar-Raajihiy: Vipi ikiwa wataacha wakategemea waadhini wengine?

Jibu: Hapana, ni wajibu katika kila msikiti. Kwa sababu kila msikiti una watu wanaomsubiri muadhini wao. Mara nyingi huwa kuna umbali baina yao kiasi cha kwamba hawawezi kumsikia muadhini wa msikiti mwingine.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31547/هل-الاذان-فرض-على-كل-مسجد
  • Imechapishwa: 02/11/2025