Swali: Nina mama ambaye ni mzee. Ana ugonjwa wa muda mrefu kwa zaidi ya miaka ishirini. Ugonjwa wake ni wa kisaikolojia. Anapopatwa na hali ya ugonjwa huwa hatambui na haswali. Lakini ugonjwa wake hupungua kwa muda fulani na hivyo huswali. Hata hivyo anapolala simwamshi kuswali ili apumzike. Je, nina dhambi kwa hilo pamoja na kuzigatia kwamba anapopata nafuu ugonjwa hurudi baada ya siku moja au mbili.
Jibu: Hili linatofautiana. Iwapo yupo katika hali ambayo hatambui, basi hatolipa. Ikiwa kutapita siku mbili, tatu au zaidi bila kutambua, basi hakuna jambo juu yake. Kwa kuwa kuwajibikiwa na ´ibaadah ndio kunakofanya hukumu zibaki. Kwa hiyo akipoteza utambuzi wake, basi hahitaji kufanya ´ibaadah.
Akipona katika baadhi ya nyakati na akili ikamrejelea, basi ataswali. Ikiwa atapona kabla ya wakati wa adhuhuri na ukafika wakati wa Dhuhr hali ya kuwa yuko na akili, ataswali Dhuhr. Ukifika wakati wa alasiri hali ya kuwa na akili, ataswali ´Aswr. Akipoteza akili kwa muda wa siku mbili, tatu, nne, chini ya hapo au zaidi, basi hatalazimishwa kulipa. Akilala usiku, inapasa kumwamsha mwishoni mwa usiku wakati wa adhaana ya Fajr. Alale mapema. Unapaswa kumwamsha kwa ajili ya Fajr. Ikiwa akili yake ipo, ataswali. Kama hana akili, basi hakuna chochote kinachomlazimu. Ukimwamsha utajua hali yake. Ikiwa itabainika kuwa akili yake ipo, basi ataamka na kuswali, na kama itabainika kuwa hana akili, basi usimtie mashaka.
Swali: Ni ipi hukumu ya kutoa swadaqah kutoka katika mali yake pia?
Ibn Baaz: Hapana, usiweke mali yake kwenye swadaqah. Mali ibaki imelindwa mpaka amri ya Allaah itimie. Akifa, itakuwa ni ya warithi. Ama akiwa hai, ibaki imelindwa isipokuwa kwa matumizi juu yake. Ikiwa utatumia kwa ajili yake, kama nguo au dawa, basi hakuna tatizo.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/29419/%D9%85%D8%A7-%D8%AD%D9%83%D9%85-%D8%B5%D9%84%D8%A7%D8%A9-%D9%88%D8%B5%D8%AF%D9%82%D8%A9%C2%A0%D8%A7%D9%84%D9%85%D8%B3%D9%86%D8%A9-%D8%A7%D9%84%D8%AA%D9%8A%C2%A0%D9%84%D8%A7-%D8%AA%D9%85%D9%8A%D9%8A%D8%B2-%D9%84%D9%87%D8%A7
- Imechapishwa: 13/08/2025
Swali: Nina mama ambaye ni mzee. Ana ugonjwa wa muda mrefu kwa zaidi ya miaka ishirini. Ugonjwa wake ni wa kisaikolojia. Anapopatwa na hali ya ugonjwa huwa hatambui na haswali. Lakini ugonjwa wake hupungua kwa muda fulani na hivyo huswali. Hata hivyo anapolala simwamshi kuswali ili apumzike. Je, nina dhambi kwa hilo pamoja na kuzigatia kwamba anapopata nafuu ugonjwa hurudi baada ya siku moja au mbili.
Jibu: Hili linatofautiana. Iwapo yupo katika hali ambayo hatambui, basi hatolipa. Ikiwa kutapita siku mbili, tatu au zaidi bila kutambua, basi hakuna jambo juu yake. Kwa kuwa kuwajibikiwa na ´ibaadah ndio kunakofanya hukumu zibaki. Kwa hiyo akipoteza utambuzi wake, basi hahitaji kufanya ´ibaadah.
Akipona katika baadhi ya nyakati na akili ikamrejelea, basi ataswali. Ikiwa atapona kabla ya wakati wa adhuhuri na ukafika wakati wa Dhuhr hali ya kuwa yuko na akili, ataswali Dhuhr. Ukifika wakati wa alasiri hali ya kuwa na akili, ataswali ´Aswr. Akipoteza akili kwa muda wa siku mbili, tatu, nne, chini ya hapo au zaidi, basi hatalazimishwa kulipa. Akilala usiku, inapasa kumwamsha mwishoni mwa usiku wakati wa adhaana ya Fajr. Alale mapema. Unapaswa kumwamsha kwa ajili ya Fajr. Ikiwa akili yake ipo, ataswali. Kama hana akili, basi hakuna chochote kinachomlazimu. Ukimwamsha utajua hali yake. Ikiwa itabainika kuwa akili yake ipo, basi ataamka na kuswali, na kama itabainika kuwa hana akili, basi usimtie mashaka.
Swali: Ni ipi hukumu ya kutoa swadaqah kutoka katika mali yake pia?
Ibn Baaz: Hapana, usiweke mali yake kwenye swadaqah. Mali ibaki imelindwa mpaka amri ya Allaah itimie. Akifa, itakuwa ni ya warithi. Ama akiwa hai, ibaki imelindwa isipokuwa kwa matumizi juu yake. Ikiwa utatumia kwa ajili yake, kama nguo au dawa, basi hakuna tatizo.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/29419/%D9%85%D8%A7-%D8%AD%D9%83%D9%85-%D8%B5%D9%84%D8%A7%D8%A9-%D9%88%D8%B5%D8%AF%D9%82%D8%A9%C2%A0%D8%A7%D9%84%D9%85%D8%B3%D9%86%D8%A9-%D8%A7%D9%84%D8%AA%D9%8A%C2%A0%D9%84%D8%A7-%D8%AA%D9%85%D9%8A%D9%8A%D8%B2-%D9%84%D9%87%D8%A7
Imechapishwa: 13/08/2025
https://firqatunnajia.com/swalah-ya-mtumzima-ambaye-anapoteza-akili-baadhi-ya-nyakati/