Swalah ya mamkuzi ya msikiti ni Sunnah katika nyakati zote

Swali: Ni ipi hukumu ya swalah ya mamkizi ya msikiti katika wakati uliokatazwa; ni wajibu au inapendeza tu?

Jibu: Swalah ya mamkizi ya msikiti ni Sunnah katika nyakati zote. Swalah ya mamkizi ya msikiti ni Rak´ah mbili katika kila wakati kwa mujibu wa maoni sahihi. Haina wakati uliokatazwa. Hata kama imamu anatoa Khutbah siku ya ijuma, mtu asiketi chini mpaka aswali Rak´ah mbili.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/30920/ما-حكم-تحية-المسجد-في-وقت-النهي
  • Imechapishwa: 16/09/2025