Swalah ya kuomba mvua jumatatu na alkhamisi?

Swali: Je, kumepokelewa Hadiyth juu ya swalah ya kuomba kuteremshiwa mvua kuifanya siku ya jumatatu au alkhamisi?

Jibu: Sitambui chochote katika hayo. Swalah ya kuomba kuteremshiwa mvua inafaa wakati wowote; siku ya jumatatu, jumamosi, jumapili, jumanne na ijumaa. Vivyo hivyo hata siku ya ijumaa. Lakini siku ya jumatatu na alkhamisi ni siku mbili ambazo matendo yanaonyeshwa kwa Allaah. Ndio maana Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akipendekeza kuzifunga siku hizo.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (22)
  • Imechapishwa: 24/10/2021