Swalah ya ghaibu kwa asiyekuwa an-Najaashiy

Swali: Je, imethibiti kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimswalia mtu mwengine swalah ya ghaibu mbali na an-Najaashiy swalah ya jeneza?

Jibu: Hapana, haikuthibiti. Kwa ajili hiyo wanachuoni wamesema kuwa ni jambo ambalo halikusuniwa kwa mwengine. Kwa sababu an-Najaashiy (Rahimahu Allaah) alikufa katika mji ambao hakuna yeyote wa kumswalia. Ana sifa maalum juu ya kitendo hichi. Allaah ndiye mjuzi zaidi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (15) https://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/Umdah-24-11-1434_0.mp3
  • Imechapishwa: 01/09/2019