Swalah ya ´Aswr baada ya kujua kuwa manjano

Swali: Baada ya jua kuwa manjano – je, swalah ya ´Aswr inatekelezwa au inalipwa?

Jibu: Inatekelezwa.

Swali: Je, anatakiwa kuilipa baada ya kutoka wakati wake?

Jibu: Atailipa, ndio salama zaidi kwa ajili ya kutoka kwenye makinzano ya wanazuoni. Vinginevyo ni batili. Lakini ikiwa atailipa kwa ajili ya kutoka kwenye makinzano, basi ni jambo zuri. Vinginevyo halazimiki kuilipa, kwa sababu alichelewesha kwa makusudi, isipokuwa kwa kutubia. Hivyo basi anatubia kwa Allaah (´Azza wa Jall) na kujirekebisha.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/25302/ما-حكم-صلاة-العصر-بعد-اصفرار-الشمس
  • Imechapishwa: 27/02/2025