Swalah ya ambaye hakupandisha maji puani

Swali: Niliamka kwa ajili ya swalah ya Fajr nikiwa nimechelewa, huku watu msikitini wakiwa tayari wameshaswali. Nilitawadha, kisha nikaenda msikitini na nikawakuta wanaswali na hivyo nikajiunga nao. Nilipokuwa katika Rak´ah ya pili nikakumbuka kwamba nilikuwa sijaingiza maji puani. Ni ipi hukumu ya swalah yangu?

Jibu: Kupandisha maji puani ni wajibu katika wudhuu´ kwa mujibu wa yale yaliyothibiti katika mwenendo wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na amri yake aliposema:

“Mwenye kutawadha basi apandishe maji puani.”[1]

Amesema tena (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Mwenye kutawadha basi apandishe maji puani.”

Mtu ambaye hakupandisha maji puani, basi wudhuu´ wake si sahihi. Kwa hiyo ni wajibu kwako kurudia wudhuu´ na kuswali tena swalah hiyo.

[1] al-Bukhaariy (161-162) na Muslim (01/46).

  • Muhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (5/209)
  • Imechapishwa: 01/11/2026