Ni lazima kuingiza kidole mdomoni wakati wa kusukutua mdomo?

Swali: Je, wudhuu´ wa mtu huwa batili ikiwa atakusukutua bila kuingiza kidole chake mdomoni? Kwa sababu imesemekana kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akisukutua huku akiingiza kidole chake mdomoni. Je, Hadiyth hiyo ni Swahiyh?

Jibu: Wudhuu´ unasihi hata ikiwa mtu hakukiingiza kidole chake mdomoni wakati wa kusukutua mdomo. Ama kuhusu Hadiyth hiyo ameipokea Imaam Ahmad kwa cheni ya wapokezi dhaifu.

  • Muhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (5/208)
  • Imechapishwa: 01/11/2026