Kusukutua mdomo na kupandisha maji puani au kuosha uso kwanza?

Swali: Katika wudhuu´, je, kuosha uso kunapaswa kutangulia kusukutua na kupandisha maji puani, au kusukutua na kupandisha maji puani kunapaswa kutangulia kuosha uso? Hili limezua mjadala baina ya watu wawili ambapo mmoja anasema kwamba uso unapaswa kuoshwa kwanza, kisha kusukutua na kupandisha maji puani, huku mwingine akisema kwamba kusukutua na kupandisha maji puani kunapaswa kufanywa kwanza kabla ya kuosha uso?

Jibu: Lililo bora kwa mwenye kutawadha aanze kwa kusukutua na kupandisha maji puani kabla ya kuosha uso, kwa kufuata mwenendo wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kwa kuwa wanazuoni wamekubaliana kwamba ni jambo linalopendekezwa kutanguliza kusukutua na kupandisha maji puani kabla ya kuosha uso. Hata hivyo ikiwa mtu ataanza kwa kuosha uso kabla ya kusukutua na kupandisha maji puani, wudhuu´ wake ni sahihi.

  • Muhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (5/207-208)
  • Imechapishwa: 01/11/2026