Swali: Ni mara ngapi kichwa kinapaswa kupanguswa wakati wa wudhuu´? Afanye nini ikiwa mtu ametawadha nyumbani, kisha akaenda msikitini na akakumbuka kwamba hakupangusa kichwa chake?
Jibu: Ni wajibu kupangusa kichwa mara moja wakati wa wudhuu´. Mtu ambaye ametawadha kisha akasahau kupangusa kichwa basi ni wajibu kwake kurudia wudhuu´ ikiwa umeshapita muda mrefu, kwa sababu kufuatana kwa viungo vya wudhuu´ bila kukatiza muda mrefu ni wajibu. Lakini ikiwa atakumbuka mara moja, basi anapaswa kupangusa kichwa, kisha aoshe miguu tena.
- Muhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (5/212-213)
- Imechapishwa: 01/11/2026
Swali: Ni mara ngapi kichwa kinapaswa kupanguswa wakati wa wudhuu´? Afanye nini ikiwa mtu ametawadha nyumbani, kisha akaenda msikitini na akakumbuka kwamba hakupangusa kichwa chake?
Jibu: Ni wajibu kupangusa kichwa mara moja wakati wa wudhuu´. Mtu ambaye ametawadha kisha akasahau kupangusa kichwa basi ni wajibu kwake kurudia wudhuu´ ikiwa umeshapita muda mrefu, kwa sababu kufuatana kwa viungo vya wudhuu´ bila kukatiza muda mrefu ni wajibu. Lakini ikiwa atakumbuka mara moja, basi anapaswa kupangusa kichwa, kisha aoshe miguu tena.
Muhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (5/212-213)
Imechapishwa: 01/11/2026
https://firqatunnajia.com/amekumbuka-kuwa-hakupangusa-kichwa-chake/