Kuosha njia ya haja kubwa baada kuamka usingizini na baada ya kutokwa na upepo

Swali: Ikiwa nimetawadha, kisha upepo ukatoka kwenye njia yangu ya haja kubwa – je, ni wajibu kwangu kuosha njia ya haja kubwa kabla ya kutawadha tena? Je, pia ni wajibu kuosha njia ya haja kubwa baada ya kuamka kutoka usingizini?

Jibu: Ikiwa hali ni kama ulivyoeleza, si wajibu wala si Sunnah kwako kuosha njia ya haja kubwa kwa sababu ya kutoka kwa upepo kabla ya kutawadha tena. Hukumu ni hiyohiyo baada ya kuamka kutoka usingizini.

  • Muhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (5/215)
  • Imechapishwa: 01/11/2026