Swali: Ni ipi hukumu ya maji yaliyonyakuliwa kwa dhuluma ikiwa mtu atatawadha kwa kutumia maji hayo? Ni ipi hukumu ya vazi lililonyakuliwa kwa dhuluma ikiwa mtu ataswali akiwa amelivaa? Je, kuna tofauti baina ya hali hizi mbili na mtu kuhiji kwa kutumia mali ya haramu?

Jibu: Uporaji ni haramu kwa maafikiano ya waislamu, kwa sababu ni dhuluma na dhuluma ni giza siku ya Qiyaamah. Mtu aliyenyakua maji kisha akatawadha kwa ajili ya swalah, akanyakua vazi kisha akaswali akiwa amelivaa au akanyakua mali kisha akahiji kwa kutumia mali hiyo, basi wudhuu´ wake, swalah yake na Hajj yake vyote ni sahihi kwa maoni yenye nguvu zaidi ya wanazuoni. Hata hivyo ni wajibu kwake kutubia kwa Allaah kutokana na jambo hilo.

  • Muhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (5/216)
  • Imechapishwa: 01/11/2026