Swalah ya aliyetia wudhuu´ kwa maji ya wizi

Swali: Je, twahara inasihi kwa maji yaliyoporwa?

Jibu: Ni haramu kuyatumia maji yaliyoporwa, si kwa sababu si safi. Maji ni safi lakini hayafai. Umeyachukua kutoka kwa mmiliki wake pasi na haki.

Swali: Kwa hiyo inasihi kutawadha nayo?

Jibu: Mtazamo sahihi ni kwamba twahara inasihi. Kwa sababu uharamu sio kwa sababu sio  safi, bali ni kwa ajili ya dhuluma. Ni kama ambavyo kwa mujibu wa maoni sahihi ni kwamba swalah inasihi juu ya ardhi iliyoporwa, si kwa sababu inajuzu kufanya hivo, bali ni kwa sababu yametimia masharti ya twahara. Hata hivyo yeye ni dhalimu kwa kuyapora na kuyanyakua na kuchukua mali bila ya haki. Yeye ataingia hatiani kwa hili.

Swali: Wale wenye kuona kuwa twahara haisihi wamejengea hoja kwa Hadiyth isemayo:

“Hakika damu yenu na mali zenu ni haramu kwenu kama ilivyo siku hii, katika mwezi huu, katika mji wenu huu.”[1]

Jibu: Ni haramu kwenu, lakini twahara ni sahihi. Kwa sababu ni maji safi aliyotawadha kwayo na kwa ajili hiyo imesihi. Lakini amedhulumu kwa jambo hilo na twahara haibatiliki. Ni kama anayeswali juu ya ardhi iliyoporwa; swalah yake inasihi ilihali yeye ni mwenye kupewa dhambi. Wanazuoni wametofautiana juu ya suala hili, hata hivyo haya ndio maoni yenye nguvu zaidi.

Swali: Ametumia dalili kwa Hadiyth juu ya kwamba twahara haisihi?

Jibu: Inafahamisha juu ya uharamu peke yake.

[1] al-Bukhaariy (1739) na Muslim (1218).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24684/هل-تصح-الطهارة-بالماء-المغصوب
  • Imechapishwa: 25/11/2024