Swali: Niliswali mara moja katika msikiti wao (Shiy´ah waliochupa mipaka) bila kujua hilo. Je, swalah yangu ni sahihi?

Jibu: Swalah yake si sahihi ikiwa imamu wa msikiti ni miongoni mwao, basi si sahihi.  Inabidi airudie swalah yake. Swalah nyuma ya kafiri haisihi. Swalah inasihi nyuma ya fasiki, si nyuma ya kafiri. Wao wanawaomba watu wa nyumbani kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), wanamuomba uokozi ´Aliy, Faatwimah, al-Hasan na al-Husayn. Aidha wanadai kuwa wanajua ghaibu na wanawatukana Maswahabah. Hao ni miongoni mwa viongozi wa ukafiri.

Swali: Ni ipi hukumu ya swalah zao ambapo wanakusanya Dhuhr na ´Aswr, Maghrib na ´Ishaa?

Jibu: Hilo ni miongoni mwa Bid´ah zao na upotofu wao. Haijuzu kukusanya Dhuhr na ´Aswr wala Maghrib na ´Ishaa isipokuwa kunapokuwa udhuru unaokubalika katika Shari´ah kama mfano wa maradhi au safari. Ama kukusanya bila udhuru ni batili na haijuzu.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/30989/ما-حكم-الصلاة-وراء-غلاة-الشيعة
  • Imechapishwa: 20/09/2025