Swali: Ni ipi hukumu ya kuswali nyuma ya imamu anayefanya makosa ya wazi kabisa?

Jibu: Hili linahhitaji ufafanuzi: Ikiwa makosa hayo yanabadilisha maana, basi anatakiwa kuonywa mpaka arekebishe. Aidha haijuzu kuswali nyuma yake iwapo hatoweza kurekebisha makosa hayo. Lakini kama makosa hayabadilishi maana na maana iko wazi, basi hilo halidhuru. Hata hivyo inatakiwa mtu ajitahidi katika Qur-aan ili asome kwa usahihi, hili ndilo limewekwa katika Shari´ah. Lakini kama makosa hayabadilishi maana, haidhuru swalah. Mfano wa makosa hayo ni:

الحمدَ لله رب العالمين * الرحمنُ الرحيم

”Himdi zote njema anastahiki Allaah, Mola wa walimwengu. Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu.”

Makosa haya hayabadilishi maana.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31003/ما-حكم-الصلاة-خلف-امام-يلحن-لحنا-جليا
  • Imechapishwa: 21/09/2025