Swalah ndani ya nguo zenye manii

Swali: Ni ipi hukumu ya kuswali ndani ya nguo yenye athari ya manii?

Jibu: Manii ni masafi. Mtu akiswali kwenye nguo zenye manii, swalah yake ni sahihi. Ni mamoja alifanya hivo kwa makusudi au kwa kusahau. Ikitokea ameswali na nguo yenye mkojo kwa kusahau au ni mjinga na hakujua isipokuwa baada ya kumaliza kuswali, basi swalah yake ni sahihi.

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/371)
  • Imechapishwa: 19/04/2026