Swalah ndani ya mavazi yenye mikono mifupi

Swali: Ni ipi hukumu ya kuswali kwenye nguo zenye mikono mifupi kwa mwanaume?

Jibu: Hapana vibaya. Mwanaume anaweza kuswali akiwa amevaa nguo ambazo zinaonyesha nusu ya mkono wake, mkono wake wote au hata bega lake lote, kwani hayo sio uchi. Hapo ni pale ambapo ataswali ndani ya nguo ya chini na juu ya mabega yake kuna kitu, hilo linatosha. Uchi wa mwanaume ndani ya swalah si mkono wake wala mguu wake, bali ni kutoka kitovuni hadi magotini, pamoja na kufunika moja ya mabega mawili. Ama mwanamume, sehemu zake za siri ndani ya swalah ni kuanzia kitovu hadi goti, huku moja ya mabega likiwa limefunikwa.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (29/220)
  • Imechapishwa: 26/02/2026