Swalah ndani ya mavazi yenye kubana kwa wanaume

Swali: Ni ipi hukumu ya kuswali kwa nguo za kubana kwa wanaume? Je, anaweza kuwaswalisha watu anayezivaa?

Jibu: Nguo za kubana zinachukiza kwa wanaume na wanawake wote. Linalopaswa ni nguo ziwe za wastani; si za kubana zinazoonyesha ukubwa wa viungo visivyotakiwa kuonekana, wala si pana kupita kiasi, bali ziwe katikati ya hayo mawili. Kuhusu swalah ni sahihi ikiwa nguo hizo zinafunika ipasavyo, lakini inachukiza kwa muumini wa kiume kuvaa mavazi ya kubana, na vivyo hivyo kwa muumini wa kike. Vazi liwe la wastani kati ya kubana na kupana. Hilo ndilo linalopaswa.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (29/220)
  • Imechapishwa: 26/02/2026