Swali: Ni ipi hukumu ya kuswali na barakoa na vifuniko vya mikono?

Jibu: Hakuna neno kufanya hivo.

Swali: Tunafanya kazi kliniki na pindi tunaswali mkusanyiko tunasimama mita moja kati ya mtu mmoja na mwingine na imamu anasimama mbele yetu. Je, swalah ni sahihi?

Jibu: Hakuna tatizo kufanya hivo.

Swali: Baadhi ya wagonjwa wa corona hawawezi kutawadha na hivyo wanalazimika kufanya Tayammum. Lakini kunachelewa vipumuaji vikaathiriwa na ule udongo. Ni ipi hukumu ya twahara katika hali hii?

Jibu: Ikiwa Tayammum inasababisha madhara, basi mgonjwa ataswali kama alivyo.

Swali: Je, inafaa kwa watunzaji wa afya wanaowaangalia wagonjwa wa corona ambao wamevaa mavazi ya kinga kufanya Tayammum ikiwa wanapata uzito wa kuyavua yale mavazi ya kinga?

Jibu: Ikiwa hawawezi kuyajua au wanadhurika kufanya hivo, basi waswali vile walivyo.

Swali: Baadhi ya nyakati watunzaji wa afya wanaweza kuingia katika hali ya dharurah kwa ajili ya kumwokoa mgonjwa kuangamia na hivyo wasiweze kuswali ndani ya wakati. Ni ipi hukumu ya hilo?

Jibu: Waswali pale watapoweza ijapo ni baada ya kutoka wakati wake.

Swali: Mgonjwa wa corona akiwa hana wudhuu´ na yuko sehemu ambayo hakuna choo na wakati huohuo anahitajia kuswali swalah ya faradhi. Hata hivyo anadhurika kutoka maeneo alipo. Ajisafishe na kuswali vipi?

Jibu: Aswali vile alivyo. Kama anaweza kujisafisha kwa maji, basi ni lazima kwake kufanya hivo. Vinginevyo afanye Tayammum. Asipoweza kutawadha wala kufanya Tayammum, basi ataswali vile alivyo.

Swali: Pindi wagonjwa wa corona wanapolazwa katika chumba cha dharurah basi watunzaji wa afya hulazimika kuvaa mavazi ya kinga, jambo ambalo linapelekea kuchelewesha matibabu kwa dakika kadhaa. Baadhi ya watunzaji wa afya wanakereka kwa hilo na wanahisi kuwa wanafanya mapungufu. Ni ipi hukumu ya hilo?

Jibu: Hakuna neno.

Swali: Madaktari na watunzaji wa afya wanajiweka khatarini pindi wanapowatibu wagonjwa. Mna chochote cha kusema juu ya hilo?

Jibu: Wanatakiwa kusubiri na kutaraji malipo kutoka kwa Allaah kwa ile kazi wanayofanya, kwa sababu wanawanufaisha ndugu zao.

Swali: Watunzaji wa afya wanaowatunza wagonjwa wa corona wanaacha kuwatembelea wazazi wao ili wasije kuwaambukiza. Je, kunazingatiwa ni utovu wa nidhamu?

Jibu: Hakuzingatiwi ni utovu wa nidamu.

´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Muhammad Aalush-Shaykh

Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan

Muhammad bin Hasan Aalush-Shaykh

´Abdus-Salaam bin ´Abdillaah as-Sulaymaaniy

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://twitter.com/aliftasa/status/1265757438868946945/photo/1
  • Imechapishwa: 30/05/2020