Swali: Vipi kuswali mahali ambapo kuna picha zilizotundikwa au TV inayocheza?
Jibu: Inasihi wakati wa haja. Lakini bora ni kuacha kufanya hivo. Ikiwa hakuna haja asiswali sehemu hiyo. Hata hivyo ikiwa kuna haja ni sawa. Ni kama ambavo ´Umar aliruhusu kuswali ndani ya kanisa kwa sababu ya haja. Hapana vibaya haja ikipelekea kuswali mahali ambapo zipo. Mfano mtu ambaye swalah imemkuta mahali ambapo kuna picha na asiweze kutoka mahali hapo. Mfano mwingine ni mgonjwa ambaye yuko mahali palipo picha na hana namna. Kwa msemo mwingine jambo ambalo linapelekea katika dharurah. Vinginevyo bora atoke katika kujifananisha na manaswara na mayahudi.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24576/حكم-الصلاة-في-مكان-به-صورة-او-تلفاز
- Imechapishwa: 03/11/2024
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket