Swali: Unasemaje kuhusu kufunika mabega? Je ni wajibu? Je, mabega ni sehemu ya uchi? Ikiwa ni sehemu ya uchi, ni katika aina ipi? Je, inajuzu kuyafunua?

Jibu: Imepokelewa katika Hadiyth Swahiyh ambapo amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

”Asiswali mmoja wenu ndani ya nguo hali ya kuwa hana chochote juu ya mabega yake.”

Kwa hiyo mabega si sehemu ya uchi, lakini Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliamrisha yafunikwe kama kuna uwezekano wa kufanya hivyo.

Jaabir amesema:

”Ikiwa nguo ni pana, jifunike nayo, na ikiwa ni nyembamba, basi jifunge nayo kiunoni.”

Kwa hiyo ikiwa mtu ana nguo ya juu au kanzu, basi aiweke juu ya mabega yake. Ni wajibu kufunika mabega yote mawili au moja kati yake, ingawa si sehemu ya uchi nje ya swalah. Hilo ni kutokana na maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

”Asiswali mmoja wenu ndani ya nguo hali ya kuwa hana chochote juu ya mabega yake.”

Hadiyth hii ameipokea al-Bukhaariy na Muslim.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31001/ما-حكم-ستر-العاتق-وهل-هو-من-العورة
  • Imechapishwa: 20/09/2025