Swali: Je, ni choo cha haja au ni choo cha kuogea?

Jibu: Ni choo cha haja.

Swali: Ikiwa mbele ya msimamo wa kuswali kuna choo, je, inadhuru?

Jibu: Haidhuru, akiliswali nacho kiko mbele yake haidhuru.

Swali: Je, ndani ya choo swalah inasihi?

Jibu: Swalah haisihi ndani ya choo; Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekataza, akasema:

”Ardhi yote ni msikiti isipokuwa makaburi na vyoo.”

Kwa sababu ni mahali panapodhaniwa kuwa na najisi.

Swali: Vipi ikiwa mtu amefungwa ndani ya choo na hawezi kutoka hadi wakati wa swalah ukaisha?

Jibu: Allaah amesema:

وَقَدْ فَصَّلَ لَكُم مَّا حَرَّمَ عَلَيْكُمْ إِلَّا مَا اضْطُرِرْتُمْ إِلَيْهِ

”… na ilihali ameshapambanua kwenu yale Aliyokuharamishieni isipokuwa vile mlivyofikwa na dharura.”[1]

Hivyo dharurah ina hukumu zake.

[1] 06:119

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31602/ما-المقصود-بالحمام-الذي-لا-تصح-الصلاة-فيه
  • Imechapishwa: 08/11/2025