Swalah iliyompita mtu inazingatiwa ya kulipa au ya wakati wake?

Swali: Mtu ambaye amelala na kukosa swalah au akaisahau – je, kwake hiyo swalah hiyo inahesabika kama ya kulipa au ya wakati wake?

Jibu: Ndio, ikiwa bado ipo ndani ya wakati wake, basi ni ya wakati wake. Ikiwa nje ya wakati wake, inaitwa ya kulipa. Hili ni jambo la istilahi tu. Ni jambo rahisi. Kile kinachokusudiwa ni kuharakisha kuiswali. Ni wajibu kwake kuharakisha, ni mamoja iwe inaitwa kulipa au ya wakati wake. Jambo hili ni lenye wasaa.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31572/هل-تكون-الصلاة-قضاء-ام-اداء-لمن-نام-عنها
  • Imechapishwa: 06/11/2025