Asmaa´ bint Abiy Bakr (Radhiya Allaahu ´anhaa) amesema:

”Wakati wa mapumziko ya vita mama yangu mshirikina alinijia. Nikamuuliza Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa kusema: ”Ee Mtume wa Allaah! Mama yangu amenijia hali ya kuwa ni mwenye kutaka. Je, nimuunge mama yangu?”[1] Akasema: ”Ndio, muunge mama yako.”[2]

Upokezi mwingine uliopokelewa na al-Bayhaqiy alioufanyia kichwa cha khabari kwa Hadiyth kwa kusema:

”Mlango unaozungumzia swadaqah iliyopendekezwa kuwapa washirikina na wengineo ambao matendo yao si yenye kusifiwa.”

Hapa inahusiana na swadaqah iliyopendekezwa. Ama kuhusu swadaqah ya lazima haijuzu kuwapa wasiokuwa waislamu. Mu´aadh bin Jabal (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisema katika Hadiyth inayotambulika:

”Wakikutii, basi wafunze kwamba Allaah amewafaradhishia kutoa zakaah ambayo itachukuliwa kutoka kwa matajiri wao na kupewa mafukara wao.”[3]

[1] Katika upokezi mwingine imekuja: ”Je, nimpe?”

[2] Swahiyh Sunan Abiy Daawuud (1412).

[3] al-Bayhaqiy (4/191).

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Silsilat-ul-Ahaadiyth as-Swahiyhah (6/1/630)
  • Imechapishwa: 26/06/2019