Swali: Ni ipi swadaqah bora zaidi kwa maiti?

Jibu: Ni kile kilicho wepesi: pesa, chakula au mavazi. Kwa maana nyingine kile kilicho wepesi, hata nusu ya tende:

“Jilindeni na Moto ijapo kwa kipande cha ndege.”

Swali: Je, haikutajwa kwamba swadaqah bora zaidi ni kunywesha maji?

Jibu: Hili linahitaji kuangaliwa vyema. Imepokelewa kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimwambia Sa´d bin ´Ubaadah katika kisa chake kumuusia mama yake, kwamba amuachie wasia wa kunywesha maji. Lakini sijui usahihi wa tamko hili:

“Hii ndiyo swadaqah bora zaidi; kunywesha maji.”

Hata hivyo ni ni miongoni mwa swadaqah bora zaidi. Kunywesha watu maji ni miongoni mwa swadaqah bora.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/25395/ما-افضل-الصدقة-عن-الميت
  • Imechapishwa: 09/03/2025