Sutrah kwa anayeswali jangwani

Swali: Ikiwa anayeswali yuko jangwani – je, aweke Sutrah?

Jibu: Ndiyo.

Swali: Vipi aweke fimbo?

Jibu: Fimbo, mstari au kitu chochote kilicho rahisi – kiti au jiwe.

Swali: Viatu?

Jibu: Hapana, iwe kitu kama kiti chenye urefu wa takriban dhiraa moja pungufu ya robo, kwani Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema katika Hadiyth Swahiyh:

“Swalah ya mtu muislamu hukatizwa isipokuwa ikiwa mbele yake kuna kitu mfano wa mwisho wa tandiko la mnyama wa kupanda; punda, mbwa mweusi na mwanamke.”

Hii inafahamisha ya kwamba mwisho wa tandiko la mnyama inakaribia dhiraa moja pungufu ya robo.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/28936/حكم-السترة-للمصلي-في-الصحراء
  • Imechapishwa: 13/05/2025