Suruwali – kujifananisha na maadui wa Uislamu

Swali: Ni ipi hukumu ya kuvaa suruwali?

Jibu: Ni kujifananisha na maadui wa Uislamu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yeyote mwenye kujifananisha na watu basi yeye ni katika wao.”[1]

Asipovaa kanzu juu yake, basi dogo liwezalo kusemwa ni kwamba inachukiza. Lakini akikusudia kujifananisha na maadui wa Uislamu, itakuwa haramu. Katika hali hiyo pengine kunakhofiwa juu yake ukafiri.

[1] Ahmad (5114, 5115 na 5667).

  • Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Qam´-ul-Mu´aanid, uk. 318
  • Imechapishwa: 21/05/2025