Swali: Haya mapote ya leo kama al-Ikhwaan, an-Nahdhwah na as-Suruuriyyah na mengineyo yanahesabika ni katika mapote yaliyotoka katika kundi la waislamu, Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah au ni katika kundi lililookoka na kuwepo kwake ni Kishari´ah na wanaowapa kiapo cha utiifu ni katika Ahl-us-Sunnah?

Jibu: Ama mapote haya na mengineyo hayahesabiki kuwa ni katika Ahl-us-Sunnah. Kilichobaki ni hukumu ya mmoja kwa mmoja. Hatuwezi kuhukumu moja kwa moja kwa mtu binafsi ya kwamba ametoka katika kundi lililookoka. Huenda akawa ni mjinga na hajui. Yule anayejua ulingano wa al-Ikhwaan al-Muslimuun, Suruuriyyah na makundi mengine ambayo yanakwenda kinyume na Sunnah na akalingania kwayo na akawa na kasumba juu yake, huyu tunaweza kusema ya kwamba sio katika kundi lililookoka.

  • Muhusika: ´Allâmah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://muqbel.net
  • Imechapishwa: 28/12/2024